Anyango Official Web Site

SCROLL

Jambo wapenzi wa Nyatiti!
Habari gani?Mimi naitwa Anyango.

Anyango binti wa Japani.
“Mbona msichana mjapani ana jina la kikenya?”
Najua mnajiuliza.
Ni kwasababu ya chombo hiki.
Kinaitwa Kamba Nane ama Nyatiti kwa kiluo.

Miaka ishirini iliyopita, nilisikia mziki wa Kamba Nane mjini Nairobi.
Hapo hapo nilipendezwa sana na Kamba Nane.
Sauti lake liligusa moyo yangu mno.
Nilisikia uvumi kwamba kigogo wa Kamba Nane aliishi Siaya.
Siku chache zilizofuata, nilipanda basi la Akamba mpaka Siaya.

Nilipofika, kigogo wa Kamba Nane alikuwa nyumbani.
Jina lake ni Okumu Korengo.

“Shikamoo Baba,” nilimsalimu “Nimetoka Japani.
Ningependa kujifunza kucheza Nyatiti (Kamba Nane) tafadhali.”
Mzee alinijibu.
“Ah -Ah hapana.
Haiwezikani.
Nyatiti ni mila na utamaduni wa Waluo. Chombo hiki hakiwezi kuchezwa na wanawake ama wazungu kulingana na kimila.

Hata hivyo, mimi sikuvunjika roho.
Roho yangu ilivutwa sana na Nyatiti Nikamwomba tena, na tena, na tena, na tena.

Mwishowe, alinikaribisha kuishi pamoja naye.
Lakini akaniambia.
Kufunzwa Nyatiti ni jambo tofauti sana na kukaribishwa nyumbani.
Kwanza alihitaji kuchunguza vizuri kama ni mtu dhabiti, myenyekevu, mkweli na wa bidii kabla hata kuongea kuhusu Nyatiti.

Hata hivo, maisha ya mshambani, kwangu ilianza.
“Pilepile adhi kulo adhi moto bang’e amadho kong’o.”
Yaani Kila siku nilienda kuteka maji mtoni, nilienda tutafuta kuni kichakani halafu baada ya uchovu wa siku nzima, tulikunywa pombe za kiasili.
Wakati mwingine tulikula kumbikumbi na “omena”.

Baada ya miwezi mitatu.
Mzee, kwa ghafla, alianza kunifunza kucheza Nyatiti. Alinihimiza “Piga!“ “Piga!“

Halafu mwana Nyatiti kwa jina la Anyango nyar Siaya alizaliwa.
Watu huniita Anyango nyar Kenya. Anyango nyar Okumu.
“The first female Nyatiti player in the world.”

Baada ya uchezaji wangu wa Nyatiti kuimarika, Okumu alinibariki akisema “Anyango dhi mabor gi Nyatiti.”
Maanake ni “Anyango nenda mbali na mziki huu.
Maana ya ndani nikwamba alinibariki nieneza mziki wa Nyatiti duniani kote mahali yeye mwenyewe hangefika.
Safari yetu bado inaendelea.

Erokamano baba. Erokamano Josiaya.
Erokamano Nyasaye.
Nawashukuru sana wakenya wote popote mlipo.

Kwa sababu ya ukubwa wa roho yenu.
Leo mimi niko hapa na Nyatiti.
Erokamano maduong’.
Asanteni sana.
ARIGATO!!!
‘‘An Anyango nyar Alego Karapul.
Guwok yombo jadwar ei kudho to oonge akala!”

“Mimi ni Anyango binti wa Alego Karapul. Mimi ni kama mbwa anayemshinda mwindaji mbio kwenye miiba lakini hajavalia chochote miduuni, hata viatu vya Akala.”

Anyango